Idadi kubwa ya majeruhi katika kikosi cha Yanga inamnyima usingizi kocha wa klabu hiyo Hans van der Pluijm kwani hadi mashine za mabao nazo hali ni tete
Wakati mzunguko wa pili wa Ligi ya Vodacom Tanzania unaanza Jumamosi kocha wa Yanga Hans van der Pluijm, ameoshesha kuwa nahofu baada ya kikosi chake kukabiliwa na wachezaji 11, majeruhi.
Pluijm ameiambia Goal, hali hiyo inampa wakati mgumu kwasababu Jumamosi anamchezo mgumu wa ugenini dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa uwanja wa Mkwakwani Tanga.
“Hiki nikipindi kigumu kwetu tupo katika mbio za za ubingwa na idadi kubwa ya wachezaji wangu  wa kikosi cha kwanza ni majeruhi sijui itakuwaje kwasababu ukipoteza mchezo mmoja unatoa nafasi kwa mwenzako kuongoza ligi,” amesema Pluijm.
Wachezaji waliokuwa majeruhi kwenye kikosi cha Pluijm ni Amissi Tambwe, Simon Msuva, Malimi Busungu, Vincent Bossou, Boubacar Garba, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Deogratius Munishi ‘Dida’, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na  Juma Abdul.
Balaa kubwa limeikumba Yanga ambayo hivi sasa ipo katika maandalizi makali ya kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara unaotarajia kuanza wikendi ijayo baada ya wachezaji wake kushindwa kufanya mazoezi. Timu hiyo ambayo kwa sasa inaongoza msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 39, imekumbwa na balaa la nyota wake 11 wa kutumainiwa kuwa nje ya uwanja wakisumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Hali hiyo imeonekana kuwachanganya vilivyo viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo, linaloongozwa na Mholanzi, Hans van Der Pluijm. Wachezaji hao ni Amissi Tambwe, Simon Msuva, Malimi Busungu, Vincent Bossou, Boubacar Garba, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haji Mwinyi, Deogratius Munishi ‘Dida’, Kelvin Yondani, Mbuyu Twite na  Juma Abdul.
Daktar wa timu hiyo Ally Nassor Matyza amesema anapambana na wasaidizi wake kuhakikisha baadhi ya wachezaji hao wanapona na kuwepo uwanjani Jumamosi kuikabili Coastal Union.